Tuesday 31 August 2010

Mapishi ya Biriani



Mahitaji

  • Mchele (rice 1/2 kilo)
  • Nyama (beef 1/2 kilo)
  • Vitunguu (onion 2)
  • Kitunguu swaum (garlic 1 kijiko cha chai)
  • Tangawizi (ginger 1 kijiko cha chai)
  • Maziwa mgando (yogurt 1 kikombe cha chai)
  • Hiliki nzima (cardamon 6)
  • Amdalasini nzima (cinamon stick 2)
  • Karafuu nzima (cloves 6)
  • Pilipili mtama nzima (black pepper 8)
  • Curry powder 1/2 kijiko cha chai
  • Binzari manjano (turmaric 1/2 kijiko cha chai)
  • Binzari nyembamba nzima (cumin 1/4 kijiko cha chai)
  • Chumvi (salt)
  • Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia nyama na uikaange kwa muda wa dakika 10. baada ya hapo tia tangawizi, kitunguu swaum, hiliki(4), amdalasini (1), karafuu (4), pilipili mtama (5), Curry powder, binzari manjano, binzari nyembamba na chumvi. Kisha koroga. Baada ya hapo tia yogurt na uipike mpaka ikauke kisha tia maji kidogo, funika na upunguze moto na uache ichemke kwa muda wa nusu saa.Baada ya hapo nyama itakuwa imeiva na mchuzi kubakia kidogo.Kwahiyo itatakiwa kuiipua.
Loweka mchele kwa dakika 10. kisha chemsha maji mengi kidogo katika sufuria kubwa. baada ya hapo tia hiliki (2) amdalamsini (1) karafuu(2) pilipili mtama (3) chumvi na mafuta kiasi. acha ichemke kidogo kisha tia mchele.Hakikisha maji yameufunika mchele kabisa na uuache uchemke kwa muda wa dakika 8 tu (kwani hautakiwi kuiva kabisa) kisha uipue na uchuje maji yote katika chujio. baada ya hapo chukua sufuria ya kuokea (baking pot kama unayoiona kweye picha) Kisha weka wali nusu na uusambaze sawia kisha weka mchuzi nyama na mchuzi wake pia utandaze na umalizie kwa kuweka leya ya wali uliobakia. Baada ya hapo ufunike na uweke kwenye oven kwenye moto wa 200°C kwa muda wa nusu saa.na baada ya hapo biriani litakuwa tayari kwa kuliwa.

Shukrani
Asante sana mdau Sharifa kwa recipe yako. Nimeijaribu na biriani  limetoka bomba. Nikaona ni vizuri  kuipublish recipe hii ili na wadau wengine wafaidike na namna nyingine ya kupika biriani. Na kama kuna wadau wengine wana recipe zao na wangependa kushare nasi, si vibaya kama watanitumia nami nitazipublish kwa moyo mkunjufu.
Asante sana.

Monday 30 August 2010

Mapishi ya bagia na chatney ya machicha ya nazi




Mahitaji

  • Kunde (Ila mimi nilitumia Nigerian brown beans 1/2 kilo)
  • Vitunguu maji (onion 2)
  • Pilipili (scotch bonnet pepper 2)
  • Vitunguu swaum (garlic 4 cloves)
  • Chumvi (salt)
  • Barking powder (1/2 kijiko cha chai)
  • Machicha ya nazi (grated coconut 1 kikombe cha chai)
  • Limao (lemon 1)
  • Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho
Loweka kunde usiku mzima kisha ziondoe maganda na uzitie kwenye blender pamoja na vitunguu maji, vitunguu swaum, pilipili, chumvi,barking powder na maji kiasi. Visage vitu vyote mpaka viwe laini na kisha uutoe na kuweka kwenye chujio ili uchuje maji. baada ya hapo zikaange katika mafuta mpaka ziwe za brown na uzitoe na kuziweka kwenye kitchen towel ili zichuje mafuta.Baada ya hapo saga machicha ya nazi,limao, pilipili  chumvi pamoja na maji kidogo na hapo chatney yako itakuwa tayari kwa kuseviwa na bagia.

Sunday 29 August 2010

Jinsi ya kupika Mkate wa sinia



Mahitaji

  • Unga wa mchele (rice flour 2 vikombe vya chai)
  • Sukari (sugar 3/4 ya kikombe cha chai)
  • Hamira (dried yeast 3/4  kijiko cha chakula)
  • Hiliki (cardamon powder 1/2 kijiko cha chai)
  • Ute wa yai 1(egg white)
  • Tui la nazi (coconut milk kikombe 1 na 1/2 cha chai)
  • Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Changanya unga wa mchele, hamira, hiliki na tui la nazi pamoja katika bakuli la plastic kisha koroga vizuri. Ufunike na uwache katika sehemu ya joto mpaka uumuke.(ambayo inaweza kuchukua kama dakika 30-45. Ukisha umuka tia sukari na ute wa yai kisha ukoroge vizuri. Baada ya hapo washa oven katika moto wa 200°C kisha chukua chombo cha kuokea na ukipake mafuta na umimine  mchanganyiko. Kisha utie katika oven na uoke kwa muda wa dakika 40. Hakikisha unaiva na kuwa rangi yabrown juu na chini. Na hapo mkate utakuwa tayari.

Saturday 28 August 2010

Mapishi ya Bagia dengu



Mahitaji

  • Unga wa dengu (gram flour 1/4 kilo)
  • Kitunguu kilichokatwa (onion 2)
  • Hoho (green pepper 1/2)
  • Pilipili iliokatwakatwa (scotch bonnet pepper 1/2)
  • Barking powder (1/4 ya kijiko cha chai)
  • Chumvi (salt)
  • Kitunguu swaum (garlic cloves 2)
  • Mafuta ya kukaangia (vegetable oil)
  • Binzari manjano (turmeric 1/4 ya kijiko cha chai)
Matayarisho
Changanya unga, chumvi, binzari, barking powder kwanza kisha weka maji kiasi na vitu vyote vilivyobakia (isipokuwa mafuta) na ukoroge vizuri kuhakikisha unga hauna madonge.Hakikisha unga hauwi mzito wala mwepesi sana. Kisha uache kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo choma bagia katika mafuta. Ukiwa unachoma hakikisha bagia zinakuja  juu ya mafuta na hazigandi chini. Ikitokea zinaganda chini hapo itakuwa umekosea kitu. Pika mpaka ziwe za light  brown kisha zitowe na uziweke katika kitchen towel ili zikauke mafuta na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Thursday 26 August 2010

Mapishi ya Tambi za sukari



Mahitaji
  • Tambi (spaghetti 1/2 ya packet)
  • Mafuta (vegetable oil)
  • Sukari (sugar 1/2 kikombe cha chai)
  • Hiliki (cardamon 1/2 kijiko cha chai)
  • Chumvi (salt 1/2 kijiko cha chai)
  • Tui la nazi (coconut oil 1 kikombe cha chai)
  • Maji kiasi


Matayarisho
Tia mafuta kiasi kwenye sufuria kisha ibandike jikoni (katika moto wa wastani) yakisha pata moto kiasi tia tambi na uanze kuzikaanga kwa kuzigeuzageuza kila mara mpaka zitakapokuwa za yangi ya light brown. baada ya hapo ipua na umwage mafuta ya kwenye tambi (bakiza kidogo sana kwani usipofanya hivyo tambi zitakuwa na mafuta sana) Baada ya hapo zirudishe jikoni na kisha utie hiliki, chumvi, sukari, tui la nazi na maji kiasi. Zifunike kisha ziache zichemke mpaka  maji yakauke. Baada ya hapo zigeuze na uzipike mpaka ziive. Nahapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Wednesday 25 August 2010

Mapishi ya Wali, mchicha wa nazi na nyama ya kukaanga


Mahitaji

  • Mchele (rice 1/2 kilo)
  • Mchicha uliokatwakatwa (spinach mafungu 2)
  • Nyama (beef 1/2 ya kilo)
  • Nyanya (tin tomato 1/2 ya tin)
  • Nyanya chungu ( garden egg 3)
  • Kitunguu swaum (garlic cloves 3)
  • Tangawizi (ginger)
  • Curry powder
  • Vitunguu (onion 2)
  • Limao (lemon 1)
  • Chumvi
  • Pilipili (scotch bonnet pepper )
  • Tui la nazi (coconut milk 1 kikombe cha chai)
Matayarisho
Kaanga kitunguu kikishaiva tia nyanya na chumvi. kaanga mpaka nyanya ziive kisha tia nyanya chungu,curry powder na pilipili 1 nzima, baada ya hapo tia mchicha na uuchanganye vizuri kwa kuugeuzageuza. Mchicha ukishanywea tia tui la nazi na uache lichemke mpaka liive na hapo mchicha utakuwa tayari.
Safisha nyama kisha iweke kwenye sufuria na utie chumvi, tangawizi, limao na kitunguu swaum. Ichemshe mpaka itakapoiva na kuwa laini. Baada ya hapo weka sufuria jikoni na mafuta kidogo yakisha pata moto tia vitunguu na nyama na uvikaange pamoja, kisha tia curry powder na ukaange mpaka nyama na viunguu vya brown. na hapo nyama itakuwa imeiva. Malizia kwa kupika wali kwa kuchemsha maji kisha tia mafuta, chumvi na mchele na upike mpaka uive. Baada ya hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuseviwa.

Tuesday 24 August 2010

Mapishi ya Wali maharage,mchuzi wa samaki na spinach


Mahitaji

  • Mchele (rice 1/2 kilo)
  • Maharage yaliyochemshwa (boiled red kidney beans 1 kikombe cha chai)
  • Samaki waliokaangwa ( 2 fried fish)
  • Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2 ya tin)
  • Vitunguu vilivyokatwa (onion 2)
  • Kitunguu swaum (garlic 3 cloves)
  • Tangawizi (ginger kiasi)
  • Limao (lemon 1/2)
  • Chumvi (salt)
  • Pilipili (scotch bonnet pepper 2)
  • Mafuta (vegetable oil)
  • Spinach
  • Tui la nazi (coconut milk 1 kikombe cha chai)
Matayarisho
Saga nyanya, kitunguu, tangawizi na kitunguu swaum pamoja. Tia kwenye sufuria na upike mpaka maji yakauke kisha tia curry powder, mafuta na chumvi na upike tena mpaka mchanganyiko uive kisha tia samaki na limao na maji kiasi na uache uchemke kiasi. Na hapo mchizi utakuwa tayari.
Osha na uzikate spinach kisha kaanga kitunguu na mafuta kiasi (hakikisha visiwe vya brown kisha tia spinach na chumvi. zipike kwa muda wa dakika 3-4 na hapo zitakuwa tayari zimeshaiva.
Wali: Chemsha maji kiasi kisha tia, chumvi, pilipili nzima(isikatwe) mafuta na tui la nazi. Baada ya hapo koroga na utie mchele na maharage na ufunike uache uchemke mpaka maji yakauke. Kisha geuza na ufunike tena na uuache mpaka uive. Baada ya hapo chakula chako kitakuwa tayari kwa kuseviwa.

Monday 23 August 2010

Mapishi ya Viazi, samaki na asparagus



Mahitaji

  • Viazi (potato 1/2 kilo)
  • Samaki (fish 2)
  • Asparagus 8
  • Kitunguu kilichokatwa (chopped onion 1)
  • Kitunguu swaum kilichosagwa (garlic 4 cloves)
  • Tangawizi iliyosagwa kiasi (ginger paste)
  • Limao (lemon 1)
  • Giligilani iliyokatwakatwa (chopped coriander)
  • Curry powder (kijiko 1 cha chai)
  • Chumvi (salt)
  • Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Safisha samaki na kisha uwamarinate na kitunguu swaum, tangawizi, limao na chumvi kwa muda wa nusu saa. Baada ya hapo wakaange na usiwakaushe sana kisha waweke pembeni. Chukua fry-pan kisha tia mafuta kidogo sana (kama 1/2 kijiko cha chai) kisha tia vitunguu maji na uvikaange kwa muda wa dakika 2 (kwani havitakiwi kuiva kabisa) kisha waweke samaki na uwachanganye na hivyo vitunguu. Kisha baada ya hapo tia giligilani iliyokatwa, kamulia limao na tia chumvi kidogo kisha geuzageuza ili kuchanganya vitu vyote na kisha ipua. Baada ya hapo menya na ukate viazi katika  vipande vya wastani, na kisha uvichemshe kidogo na visiive kabisa. Baada ya hapo weka sufuria jikoni kwenye moto wa wastani na utie mafuta kidogo (kama vijiko 2 vya chakula) na kisha tia viazi na uanze kuvipika kwa kuvigeuzageuza mpaka viive na kuwa rangi ya brown kisha tia chumvi kidogo, curry powder na giligilani iliyokatwa.Vipike kwa muda wa dakika mbili kisha viipue. Na baada ya hapo malizia kwa kupika asparagus. Kwanza zioshe kisha zikate kati. Baada ya hapo weka mafuta kidogo kama 1/2 kijiko katika fry-pan yakisha pata moto tia kitunguu swaum, asparagus na chumvi.Zipike kwa kuzigeuzageuza kwa muda wa dakika 5 na hapo zitakuwa zimeshaiva na tayari kwa kuliwa pamoja na samaki na viazi. Unaweza kuvisevu kwa ketchup.

Sunday 22 August 2010

Mapishi ya Pilau ya nyama ya ng'ombe na kachumbari



Mahitaji

  • Mchele (rice vikombe 3)
  • Nyama ya ng'ombe (beef 1/2 kilo)
  • Viazi mbatata (potato 3)
  • Vitunguu maji (onions 3)
  • Kitunguu swaum (garlic cloves 4)
  • Tangawizi iliyosagwa (ginger kiasi)
  • Hiliki nzima (cardamon 4)
  • Karafuu (clove 4)
  • Pilipili mtama (blackpepper 4)
  • Amdalasini (cirnamon stick 1)
  • Binzari nyembamba nzima(cumin seeds 1/2 ya kijiko cha chai)
  • Binzari nyembamba ya kusaga (ground cumin 1 kijiko cha chai)
  • Chumvi (salt)
  • Mafuta (vegetable oil)
  • Nyanya (fresh tomato 3)
  • Limao (lemon 1)
  • Pilipili (chilli 1)
  • Hoho (green pepper)
Matayarisho
Chemsha nyama na chumvi na nusu ya limao mpaka iive kisha weka pembeni. Baada ya hapo andaa vitu vya pilau kwa kuloweka mchele kwenye maji kwa muda wa dakika 10.Menya na kukatakata vitunguu na viazi kisha weka pembeni na pia chemsha maji ya moto na uweke pembeni. Baada ya hapo weka sufuri jikoni na tia mafuta kiasi . Yakisha pata moto tia vitunguu na uvikaange mpaka viwe vya rangi ya kahawia na kisha uitie nyama na ikaange mpaka ipate rangi ya bown pia. Baada ya hapo tia kitunguu swaum na tangawizi na uikoroge vizuri kisha iache ikaangike kwa muda wa dakika 2 kisha tia spice ambazo ni Binzari nyembamba ya unga, hiliki,karafuu, amdalasini na pilipili mtama na viazi. Baada ya hapo unatakiwa ugeuze geuze mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia mchele na ugeuzege mpaka uchanganyike na viungo. Baada ya hapo tia chumvi na maji ya kutosha na ukoroge vizuri kisha funika na uache uchemke katika moto wa wastani. Maji yakikaribia kukauka tia binzari nyembamba nzima na ufunike uache mpaka maji yakauke kabisa. maji yakisha kauka ugeuze na ufunike tena na uuache mpaka uive.
Baada ya hapo andaa kachumbali kwa  kukatakata vitunguu katika bakuli na kisha tia chumvi kwa ajili ya kuondoa ukali wa vitunguu. Baada ya hapo vioshe mpaka chumvi yote iishe. osha nyanya, Pilipili, hoho na kisha katakata slice nyembamba na uchanganye na vitunguu. Baada ya hapo tia chumvi, kamulia limao na uchanganye zote pamoja. Baada ya hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuliwa.

Friday 20 August 2010

Mapishi ya Beef Burger (Home-made)



Mahitaji

  • Nyama ya kusaga (mince beef 1/4 kilo)
  • Yai (egg 1)
  • Unga wa mkate (bread crumbs 2 vijiko vya chai)
  • Kitunguu swaum kilichosagwa (garlic paste 1/2 kijiko cha chai)
  • Kitunguu maji (onion 1)
  • Tangawizi iliyosagwa (ginger paste 1/2 kijiko cha chai)
  • Nyanya (fresh tomato 1)
  • Tango (cucumber 1/4)
  • Lettice
  • Chumvi (Salt 1/2 kijiko cha chai)
  • Ketchup
  • Mayonnaise
  • Burger bun (mikate ya burger 3)
Matayarisho
Weka nyama kwenye bakuli kisha tia chumvi, yai, unga wa mkate kitunguu swaum,tangawizi na pia kitunguu maji (kikate vipande (cubes ndogo ndogo) na kisha uichanganye vizuri na uitawanyishe katika madonge 3 Baada ya hapo iache imarinate kwa muda wa dakika 30 na itakuwa tayari kwa kupikwa. Unaweza kuipika katika jiko la mkaa kwa kuweka wavu wa kuchomea nyama katika moto wa wastani, Pika upande mmoja mpaka uive na kisha ugeuze upande wa pili na pia uupike mpaka uive
Ikiwa hauna jiko la mkaa unaweza kutia kwenye oven na uigrill kwa muda wa dakika 15 kila upande katika moto wa wastani mpaka hapo baga itakapoiva.
Baada ya hapo andaa mkate wa burger kwa kuukata kati kisha katakata (slice) tango, kitunguu,nyanya na lettice.Kisha anza kuvipanga kwenye mkate wa burger kwa kuweka lettice chini kisha tango,nyanya, vitunguu na kisha burger yenyewe. Baada ya hapo tia mayonnaise na ketchup juu ya burger na upange tena vitunguu, nyanya, tango na lettice. Baada ya hapo weka mkate wa burger kwa juu na burger itakuwa tayari kwa kuliwa.

Thursday 19 August 2010

Mapishi ya Ndizi na samaki



Mahitaji

  • Ndizi laini (Matoke 6)
  • Viazi mbatata (potato 3)
  • Samaki wabichi wa wastani ( Fresh tilapia 2)
  • Kitunguu swaum (garlic 6 cloves)
  • Tangawizi (fresh ground ginger vijiko 2 vya chai)
  • Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2 kopo)
  • Vitunguu (onion 1)
  • Pilipili (chilli 1 nzima)
  • Chumvi (salt to your taste)
  • Mafuta (vegetable oil)
  • Limao (lemon 1/2)
  • Curry powder (1/2 kijiko cha chai)
Matayarisho
Safisha samaki kisha wakate vipande vitatu. Wakaushe maji kisha wamarinate na kitunguu swaum,tangawizi, chumvi, na limao kwa muda wa masaa 2. baada ya hapo waoke kwenye oven kwa muda wa dakika 30. baada ya hapo andaa ndizi na viazi kwa kuzimenya na kuziosha kisha ziweke pembeni. Kisha katakata vitunguu maji, Tangawizi, vitunguu swaum na nyanya kisha  vitie kwenye blenda na usage mpaka mchanganyiko usagike vizuri. Baada ya hapo tia mchanganyiko katika sufuria na ubandike jikoni, acha uchemke mpaka maji yote yakauke. Maji yakisha kauka punguza moto na utie mafuta, curry powder, pilipili na chumvi. Kaangiza mpaka mchanganyiko uive na baada ya hapo tia viazi na maji kiasi na uache viazi vichemke mpaka vikaribie kuiva kisha tia ndizi na samaki na ufunike. Pika mpaka ndizi na viazi viive. Baada ya hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuseviwa.

Wednesday 18 August 2010

Mapishi ya Ugali, dagaa (wabichi) na matembele



Mahitaji



  • Dagaa wabichi  (Fresh anchovies packet 1)
  • Unga wa ugali (corn meal flour 1/4 kilo) (unaweza kutumia unga wa choice uipendayo)
  • Matembele ya kukaushwa (dried sweet potato leaves, handful)
  • Nyanya ya kopo (tin tomato 1)
  • Kitunguu maji (onion 2)
  • Limao (lemon 1/4)
  • Pilipili mbuzi nzima bila kukata (scotch bonnet pepper1, do not chop)
  • Chumvi (salt 1/2 ya kijiko cha chai)
  • Mafuta (vegetable oil) 
  • Hoho (green pepper 1)
  • Kitunguu swaum (garlic 5 cloves)
  • Tangawizi (ginger 1 kijiko cha chai)
  • Binzari ya curry (Curry powder 1/2 kijiko cha chai)
Matayarisho
Safisha dagaa kwa kutoa vichwa na utumbo kisha waoshe na uwakaushe na kitchen towel na uwaweke pembeni. Baada ya hapo katakata, vitunguu na hoho kisha weka pembeni. Baada ya hapo weka sufuria jikoni na utie mafuta yakisha pata moto tia dagaa na uwakaange mpaka wawe wa brown, kisha tia kitunguu swaum,curry powder na tangawizi, kaanga kidogo kisha malizia kwa kutia vitunguu maji, hoho,pilipili,chumvi na ukamulie limao. Kaanga kwa muda wa dakika 3-4 na hakikisha vitunguu na hoho haviivi sana na hapo dagaa watakuwa tayari.

Baada ya hapo yaoshe na uyaloweka matembele (kama ni makavu) kwa muda wa dakika 15, Kisha yatoe na uyaweke kwenye sufuria pamoja na kitunguu, nyanya, chumvi ,kamulia limao kidogo, pilipili na maji kiasi. acha matembele yachemke kwa muda wa dakika 20 na uhakikishe yameiva kwa kuwa laini. Baada ya hapo yapike mpaka maji yote yakauke na mafuta yatok na hapo matembele yatakuwa tayari.

Ukisha maliza kupika dagaa na matembele andaa chungu cha ugali. Kwanza unatakiwa kuchemsha maji ya moto, kisha koroga pembeni unga kiasi katika maji ya baridi na utie kwenye maji yanayochemka, Fanya kama unatengeneza uji, uji wa ugali ukishachemka tia unga na uanze kuusonga mpaka ugali uive. Ukisha iva pakua na usevu na mboga tayari kwa kuliwa. 

Mapishi ya Supu ya samaki,viazi na broccoli

Mahitaji

  • Samaki mbichi 1
  • Viazi mbatata (potato 2)
  • Broccoli (kiasi)
  • Nyanya (Fresh tomato 1)
  • Kitunguu (onion 1/2)
  • Chumvi (salt 1/4 kijiko cha chai)
  • Limao (lemon 1/4)
  • Pilipili (chilli 1 nzima)
  • Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Safisha samaki na umkate vipande 3. Menya viazi na kisha vikate vipande vya wastani, Pia katakata nyanya, kitunguu na broccoli kisha weka pembeni. Chukua sufuria kisha tia viazi na maji kiasi kisha vichemche kiasi karibia kuiva. Baada ya hapo tia samaki, kitunguu, nyanya, broccoli, chumvi limao,pilipili na mafuta kidogo. Acha supu ichemke mpaka viazi na samaki viive kisha supu itakuwa tayari.

Monday 16 August 2010

Mapishi ya Biriani la nyama ya ng'ombe



Mahitaji

  • Nyama ya ng'ombe (beef 1/2 kilo)
  • Mchele (rice 1/2 kilo)
  • Vitunguu (onion 2)
  • Viazi (potato 2)
  • Vitunguu swaum (garlic 3 cloves)
  • Tangawizi (ginger)
  • Nyanya ya kopo (tomato 1/2 ya tin)
  • Curry powder (1/2 kijiko cha chai)
  • Binzari nyembamba ya kusaga (cumin 1/2 kijiko cha chai)
  • Binzari manjano (tarmaric 1/2 kijiko cha chai)
  • Mafuta (vegetable oil)
  • Chumvi (salt)
  • Rangi ya chakula (food colour)
  • Giligilani (fresh coriander)
  • Maziwa ya mgando (yogurt kikombe 1 cha chai)
  • Hiliki nzima (cardamon 3cloves)
  • Karafuu (clove 3)
  • Pilipili mtama nzima (black pepper 5)
  • Amdalasini (cinamon stick 1)
Matayarisho
Katakata nyama kisha ioshe na uiweke kwenye sufuria kisha tia kitunguu swaum, tangawizi, nyanya, curry powder, binzari zote, chumvi na maziwa ya mgando kisha bandika jikoni ichemke mpaka nyama iive na mchuzi ubakie kidogo.Baada ya hapo kaanga viazi na uweke pembeni, kisha kaanga vitunguu na mafuta mpaka viwe ya brown na kisha uvitie viazi vitunguu, na mafuta yake katika nyama. Koroga na uache uchemke kidogo kisha ipua na utie fresh coriander iliyokatwa na hapo mchuzi wako utakuwa tayari.
Baada ya hapo loweka mchele wako kwa muda wa dakika 10, kisha chemsha maji yatie chumvi, hiliki, karafuu, pilipili mtama na abdalasin na mafuta. Yakisha chemka tia mchele na uache uchemke mpaka ukauke maji yakisha kauka tia rangi ya chakula na uanze kugeuza ili ichanganyike na wali wote. Baada ya hapo ufunike na uache mpaka uive. Na baada ya hapo biriani litakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Chapati za Kusukuma





Mahitaji
  • Unga wa ngano (plain flour 1/2 of kilo)
  • Siagi (butter vijiko 2 vya chakula)
  • Yai (egg 1)
  • Chumvi (1/2 ya kijiko cha chai)
  • Hiliki (ground cardamon 1/4 ya kijiko cha chai)
  • Maji ya uvuguvugu (warm water)
  • Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho
Weka unga wa ngano katika bakuli la kukandia, kisha tia chumvi na  hiliki na uchanganye kwanza, baada ya hapo tia siagi na uichanganye vizuri na unga mpaka ipotee. Baada ya hapo tia tena yai na uchanganye vizuri. Mchanganyiko ukishachanganyika vizuri sasa unaweza kutia maji ya uvuguvugu kidogo, kidogo huku ukiwa unauchanganya ili kupata donge. Baada ya hapo anza kukanda hilo donge mpaka mabuje yote yapotee na unga uwe mlaini, ambapo itakuchukua kama dakika 15. Baada ya hapo tawanyisha unga katika madonge ya wastani (yasiwe makubwa sana au madogo sana) Ukimaliza hapo, andaa kibao cha kusukumia chapati kwa kukitia unga kidogo ili chapati isinatie kwenye kibao. Sukuma donge moja la chapati mpaka liwe flat na kisha weka kijiko kimoja cha mafuta na usambaze. ukisha maliza ikunje (roll). Fanya hivyo kwa madonge yote yaliyobakia.
Baada ya hapo andaa chuma cha kuchomea (fry-pan) katika moto wa wastani. Kisha anza kusukuma chapati (ni vizuri ukaanza na zile ulizozikunja mwanzo ili kuzipa nafasi zile za mwisho ziweze kulainika) ukiwa unasukuma hakikisha zinakuwa flat (na zisiwe nene sana au nyembamba sana) Ukishamaliza hapo tia kwenye chuma cha kuchomea. Acha iive upande mmoja then igeuze upande wa pili. Tia mafuta ama kijiko kimoja kikubwa upande wa chini wa chapati na uanze kuukandamiza kwa juu uku ukiwa unaizungusha. fanya hivyo uku ukiwa unaigeuza kuiangalia kwa chini ili isiungue. ikishakuwa ya brown, geuza upande wa pili na urudie hivyohiyvo mpaka chapati iive. Rudia hii process kwa chapati zote zilizobakia.

Siri ya chapati kuwa laini ni kutia siagi au mafuta ya kutosha kipindi unazikanda na pia kuzikanda mpaka unga uwe laini.

Saturday 14 August 2010

Mapishi ya Uji wa ulezi



Mahitaji

  • Unga wa ulezi (millet flour vijiko 3 vya chakula)
  • Maziwa fresh (milk 1/2 kikombe)
  • Sukari (sugar 1/4 ya kikombe cha chai)
  • Siagi (butter kijiko 1 cha chakula)
  • Maji (vikombe 4 vya chai) (serving ya watu wawili)
Matayarisho
Chemsha maji ya uji, Kisha koroga unga na maji ya baridi kiasi na uchanganye kwenye maji ya moto yanayochemka. Endelea kukoroga mpaka uchemke ili kuhakikisha uji haupatwi na madonge. Ukishachemka tia, maziwa, sukari na butter. Kisha acha uchemke kwa muda wa dakika 10 na hapo uji utakuwa tayari.

Friday 13 August 2010

Mapishi ya Ugali na dagaa



Mahitaji

  • Dagaa (dried anchovies packet 1)
  • Unga wa ugali (corn meal flour 1/4 kilo) (unaweza kutumia unga wa choice uipendayo)
  • Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2)
  • Kitunguu maji (onion 1)
  • Limao (lemon 1/4)
  • Pilipili mbuzi nzima bila kukata (scotch bonnet pepper1, do not chop)
  • Chumvi (salt 1/4 ya kijiko cha chai)
  • Mafuta (vegetable oil) 
  • Hoho (green pepper)
Matayarisho

Chambua dagaa kwa kutoa vichwa vyao na utumbo, baada ya hapo waloeke katkika maji ya moto kwa muda wa dakika 5 na uaoshe tena katika maji ya baridi na uwakaushe uwaweke pembeni. Ukishamaliza katakata kitunguu na uandae nyanya tayari kwa upishi. Bandika sufuria ya kupikia dagaa jikoni na utie mafuta, yakishapata moto tia vitunguu pamoja na dagaa. Kaanga mpaka dagaa wawe light brown kisha tia nyanya, chumvi na pilipili. Pika nyanya mpaka ziive (ukitaka kujua kama nyanya zimeiva utaona zinatengana na mafuta) Baada ya hapo kamulia limao kidogo sana na tia pilipili hoho na zipike kama dakika mbili. kisha ipua.
Ukisha maliza kupika dagaa andaa chungu cha ugali. Kwanza unatakiwa kuchemsha maji ya moto, kisha koroga pembeni unga kiasi katika maji ya baridi na utie kwenye maji yanayochemka, Fanya kama unatengeneza uji, uji wa ugali ukishachemka tia unga na uanze kuusonga mpaka ugali uive. Ukisha iva pakua na usevu na mboga tayari kwa kuliwa.

Thursday 12 August 2010

Mapishi ya Chapati za maji



Mahitaji

  • Unga wa ngano (plain flour) ( 1/4 kilo)
  • Yai (egg 1)
  • Sukari (sugar 1/4 kikombe cha chai)
  • Chumvi (salt 1/4 kijiko cha chai)
  • Hiliki (ground cardamon 1/4 kijiko cha chai)
  • Maji kiasi
  • Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Tia unga kwenye bakuli, kisha weka sukari, chumvi, hiliki na maji kiasi. Kisha koroga mpaka mchanganyiko wako uwe mzito. Baada ya hapo tia yai na ukoroge tena. hakikisha mchanganyiko hauwi mzito sana au mwepesi sana.Baada ya hapo onja kama kila kitu kimekolea. Injika chuma cha kupikia chapati (fry-pan) jikoni  katika moto wa wastani. Baada ya hapo tia nusu kijiko cha chakula cha mafuta katika fry-pan na kisha yatandaze. Hakikisha chuma kinapata moto na weka upawa mmoja wa unga wa chapati na uutandaze mpaka uwe flat. Baada ya hapo subiri mpaka chapati ikauke juu na kisha igeuze upande wa pili tia mafuta kijiko 1 kikubwa cha chakula kwa upande wa chini na wa juu kisha uanze kuikandamiza kwa juu na kijiko ili iweze kuiva vizuri kwa chini. Ikisha kuwa ya rangi ya brown igeuze na upike upande wa pili kiasi kisha iipue na uiweke kwenye sahani yenye kitchen towel ili kukausha mafuta. Rudia hii process kwa unga wote uliobakia. Na chapati zitakuwa tayari

Wednesday 11 August 2010

Mapishi ya Ndizi mzuzu



Mahitaji

  • Ndizi tamu (plantain) 3-4
  • Tui la nazi (coconut milk) kikombe 1 cha chai
  • Sukari (sugar) 1/4 ya kikombe cha chai
  • Hiliki (Ground cardamon) 1/4 ya kijiko cha chai
  • Chumvi (salt) 1/4 ya kijiko cha chai
Matayarisho

Menya ndizi kisha zikwangue utomvu wote. Baada ya hapo zikate kati (kiurefu) na kisha kata tena kati katika kila ndizi vitoke vipande 4. baada ya hapo toa moyo wa katikai wa ndizi. Zioshe na kisha zikaushe maji na uziweke kwenye sufuria ya kupikia. Baada ya hapo tia tui la nazi, sukari, chumvi na hiliki. Ziinjike jikono na uziache zichemke uku ukiwa unalikoroga tui ili lisikatike. Baada ya dakika 10 tui la nazi litakuwa limepungua na kubaki kidogo na hapo ndizi zitakuwa zimeshaiva. Ziache zipoe na zitakuwa tayari kwa kuliwa. Zinaweza kuliwa kama mlo (main meal) au kitinda mlo (dissert) au mlo wa pembeni (side dish) haswa kwa futari.

Tuesday 10 August 2010

Mapishi ya Mandazi



Mahitaji

  • Unga wa ngano (nusu kilo)
  • Sukari (Kikombe 1 cha chai)
  • Chumvi (nusu kijiko cha chai)
  • Hamira (kijiko kimoja cha chai)
  • Yai (1)
  • Maziwa ya unga (vijiko 2 vya chakula)
  • Butter (kijiko 1 cha chakula)
  • Hiliki (kijiko1 cha chai)
  • Maji ya uvuguvugu ya kukandia
  • Mafuta ya kuchomea
Matayarisho

Tia unga kwenye bakuli kisha tia sukari, chumvi, yai, maziwa ya unga, butter na hiliki kisha uchanganye pamoja mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. Baada ya hapo tia maji ya uvuguvugu kiasi na uanze kuukanda. Ni vizuri ukaukanda kwa muda wa dakika 15 ili kuhakikisha donge lote la unga limelainika vizuri.
Baada ya hapo Tawanyishaa unga uliokwandwa katika madonge 4. Tia unga wa ngano kidogo katika kibao cha kusukumia na uanze kusukuma donge moja katika shape ya chapati na hakikisha haiwi nyembamba sana wala nene sana yani inatakiwa iwe ya wastani.Ukishamaliza kusukuma unatakiwa ukate shape uipendayo na uyatandaze katika kitu kilichopo flat na kiwe kimenyunyuziwa unga wa ngano ili kuyazuia yasigandie. Rudia hiyo process kwa madonge yote yaliyobakia. Baada ya hapo yaweke mandazi katika sehemu iliyokuwa na joto ili yaweze kuumuka (inaweza kuchukua masaa 3 kuumuka). Yakisha umuka unatakiwa uweke mafuta katika karai la kuchomea. Yakisha pata joto la kiasi unatakiwa utumbukize mandazi na unaze kuyachoma mpaka yawe ya brown. Yakisha iva yaipue na uyaweke kwenye kitchen towel iliyakauke mafuta. Yakisha poa yatakuwa tayari kwa kuliwa. 

Monday 9 August 2010

Mapishi ya Viazi utamu na kachumbari




Mahitaji

  • Viazi utamu 3
  • Nyanya 2 kubwa
  • Kitunguu
  • Tango
  • Limao
  • Chumvi
  • Pilipili
  • Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho

Menya viazi na kisha vikate katika vipande. Tia mafuta kwenye chuma cha kukaangia, yakisha pata moto tia viazi nauviache vikaangike mpaka upande mmoja uwe wa brown na kisha geuza upande wa pili na upike mpaka uwe wa brown. Vikisha iva ipua na uweke kwenye kitchen towel ili vikauke mafuta.
Kachumbali: Katakata vitunguu katika bakuli na kisha tia chumvi kwa ajili ya kuondoa ukali wa vitunguu. Baada ya hapo vioshe mpaka chumvi yote iishe. osha nyanya, Pilipili tango na kisha katakata slice nyembamba na uchanganye na vitunguu. Baada ya hapo tia chumvi, kamulia limao na uchanganye zote pamoja   .Baada ya hapo viazi na kachumbali vitakuwa tayari kwa kuliwa.

Friday 6 August 2010

Mapishi ya Mchemsho wa ndizi na nyama



Mahitaji

  • Ndizi mbichi 6
  • Nyama ya ng'ombe (nusu kilo)
  • Viazi mviringo 2
  • Kitunguu swaum
  • Tangawizi
  • Kitunguu maji
  • Nyanya 1 kubwa
  • Mafuta (vegetable oil)
  • Chumvi
  • Limao
  • Pilipili
Matayarisho

Chemsha nyama na limao, kitunguu swaum, tangawizi chumvi na maji kiasi mpaka nyama iive, Hakikisha unaiacha na supu kiasi kwa ajili ya kuwekea kwenye ndizi.Kisha katakata nyanya na vitunguu na uweke pembeni .Menya ndizi na viazi kisha zichemshe pamoja na vitunguu, nyanya, maji kidogo, mafuta  na uhakikishe haziivi kabisa. Baada ya hapo tia nyama na supu yake, pilipili mzima na chumvi na uache uchemke mpaka ndizi na viazi viive.Na baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa

Thursday 5 August 2010

Mapishi ya Wali, samaki wa nazi na kisamvu



Mahitaji

  • Mchele
  • Kisamvu kilichotwangwa
  • Samaki
  • Mbaazi
  • Nyanya chungu
  • Vitunguu
  • Nyanya ya kopo
  • Tangawizi
  • Kitunguu swaum
  • Vegetable oil
  • Curry powder
  • Tui la nazi (kopo 2)
  • Chumvi
  • Pilipili
  • Limao
Matayarisho

Safisha samaki kisha wamarineti na kitunguu swaum, tangawizi, pilipili, chumvi na limao kwa muda wa masaa 3.Baada ya hapo wakaange na usiwakaushe sana na uwaweke pembeni kwa ajili ya kuungwa.Katakata vitunguu maji, saga tangawizi na kitunguu swaum. Baada ya hapo injika sufuria ya mchuzi jikoni na mafuta kiasi ya kupikia, mafuta yakisha pata moto, tia vitunguu maji na vikaange mpaka viwe vya rangi ya brown. kisha tia kitunguu swaum na tangawizi.kaanga kidogo kisha tia nyanya ya kopo moja na ufunike. acha mpaka nyanya ziive. Kisha tia chumvi na curry powder na uache ikaangike kwa muda wa dakika 2 kisha tia samaki na nyanya chungu nakisha kamulia nusu ya limao. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia tui la nazi kopo moja na uache ichemke mpaka mchuzi uive. 

Baada ya hapo chemsha kisamvu pamoja na mbaazi  Kikisha iva, kaanga kitu na nyanya pembeni mpaka ziive kisha tia kisamvu. geuza mchanganyiko mpaka uchanganyike vizuri kisha tia tui la nazi na chumvi na aacha ichemke mpaka tui liive kisha ipua.malizia kwa kupika wali ambapo utachemsha maji kisha tia mafuta,chumvi na mchele na uupike mpaka uive kisha sevu na mboga ulizopika na mlo wako utakuwa tayari kwa kuliwa.

Wednesday 4 August 2010

Mapishi ya Tambi na nyama ya kusaga




Mahitaji

  • Tambi (Spaghetti)
  • Nyama ya kusaga
  • Kitunguu maji
  • Nyanya ya kopo
  • Kitunguu swaum
  • Tangawizi
  • Carrot
  • Hoho
  • Lemon
  • Chumvi
  • Curry powder
  • Mafuta
  • Fersh coriander
Matayarisho

Katakata vitunguu maji, carrot, hoho, kisha weka pembeni. Saga vitunguu swaum na tangawizi pamoja kisha weka pembeni. Baada ya hapo injika sufuria jikoni, tia mafuta. Yakisha pata moto tia vitunguu maji kaanga mpaka vigeuke rangi ya kahawia kisha tia kitunguu swaum na tangawizi.baada ya hapo tia nyanya ya kopo na iache ichemke mpaka iive. Baada ya nyanya kuiva tia curry powder na chumvi. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia nyama ya kusaga na uiache ichemke mpaka iive.Baada ya nyama kuiva tia Corrot na hoho na uzipike kwa muda wa dakika 2.Na baada ya hapo mboga itakuwa imeivaa, iipue na katia fresh coriander. Baada ya hapo injika sufuria yenye maji jikoni. Yaache yachemke na kisha tia chumvi na mafuta ya mzaituni (olive oil) na tambi. Acha zichemke mpaka ziive kisha zichuuje maji na chujio na baada ya hapo zitakuwa tayari kuseviwa na nyama.


Tuesday 3 August 2010

Mchemsho wa samaki na viazi



Mahitaji


  • Samaki mbichi (1)
  • Viazi mbatata (3)
  • Nyanya (1)
  • Kitunguu maji
  • Limao
  • Kitunguu saumu 
  • Tangawizi
  • Chumvi
  • Pilipili
  • Vegetable oil
Matayarisho

Safisha samaki kisha mmarinate na tangawizi, kitunguu swaum, chumvi na limao kwa muda wa masaa mawili. Baada ya hapo menya viazi na uvikate vipande vidogo kisha vioshe na viweke kwenye sufuria yenye maji kiasi kwa ajili ya kuvichemsha. Viinjike jikoni na uviache vichemke kwa dakika 7. Vikisha chemka tia samaki, katia kitunguu,pilipili, chumvi, limao, vegetable oil na nyanya na uache supu ichemke mpaka samaki na viazi vitakapoiva. baada ya hapo supu itakuwa tayari kwa kuliwa.

Monday 2 August 2010

Jinsi ya kupika Eggchop



Mahitaji

  • Mayai yaliochemshwa 4
  • Nyama ya kusaga robo kilo
  • Kitunguu swaum
  • Tangawizi
  • Limao
  • Chumvi
  • Pilipili
  • Breadcrambs
  • Carry powder
  • Binzari nyembamba ya unga
  • Yai moja bichi
  • Mafuta 

Matayarisho

Marinate nyama na pilipili, kitunguu swaum, tangawizi, limao, chumvi, carry powder, binzari nyembamba na breadcrambs pamoja. Kisha vunja yai moja bichi kwenye kibakuli na ulikoroge kisha tia kwenye mchanganyiko wa nyama.Gawanisha matonge manne kwa ajili ya kuzungushia kwenye mayai .Chemsha mayai kwa muda wa dakika 20. Yakisha iva acha yapoe na kisha yamenye maganda na uyaweke pembeni. Baada ya hapo chukua yai moja lililochemshwa na ulizungushie donge moja la mchanganyiko wa nyama. fanya hivyo kwa mayai yote yaliobakia. Baada ya hapo paka mafuta kwa nje ya hizo eggchop na kisha paka mafuta kwenye sinia la kuokea na uziokee kwenye oven kwa moto wa kawaida, kwa muda wa dakika 20.Na eggchop zako zitakuwa tayari kwa kuliwa

Sunday 1 August 2010

Mapishi ya Wali, samaki, bilinganya na spinach


Mahitaji

  • Samaki
  • Spinach
  • Bilinganya
  • Nyanya ya kopo (Kopo 1)
  • Vitunguu maji
  • Vitunguu swaumu
  • Tangawizi
  • Pilipli mbuzi
  • Chumvi
  • Limao
  • Carry powder
  • Mchele
  • Mafuta ya kupikia
  • Coriander
  • Hiliki
  • Amdalasini
  • Karafuu

Matayarisho

Osha samaki na kisha wamarinate na vitunguu swaumu, tangawizi, limao, chumvi na pilipili kwa muda wa masaa matatu. Baada ya hapo wakaange samaki na uwaweke pembeni kwa ajili ya mchuzi.
Osha spinach na kisha zikatekate na ziweke pembeni
Osha mchele na kisha uloweke kwenye maji kwa muda wa dakika kumi
Osha bilinganya kisha likatekate vipande vidogo dogo

Jinsi ya kupika

Mchuzi
Saga pamoja vitunguu maji, vitunguu saumu, tangawizi, nyanya.Kisha weka mchanganya katika sufuria na uinjike jikoni kwenye moto wa kawaida. Pika mchanganyiko mpaka ukauke kisha tia mafuta, chumvi na carry powder. pika kwa muda wa dakika kumi kisha tia samaki na tui la nazi. Acha mchuzi uchemke mpaka tui la nazi liive.kishaipua na tia coriander

Spinach
Kaanga vitunguu maji na mafuta, baada ya hapo tia spinach na chumvi acha ziive kidogo kisha ipua tayari kwa kuliwa.

Mabilinganya
Kaanga vitunguu maji na mafuta mpaka viwe vya brown kisha tia nyanya. Acha ziive kisha tiai mabilinganya na chumvi. Yakishaiva ipua weka pembeni tayari kwa kuliwa.

Wali
Chemsha maji ya wali kwenye sufuria, kisha tia hiliki, pilipili mtama mzima, karafuu na amdalasini, chumvi na mafuta. Kisha tia mchele na uufunike na uache uchemke mpaka utakapokauka maji. Geuza na uache mpaka uive. Kisha ipua. Tayari kwa kuliwa